MAONO YETU

MAONO YA HUDUMA YA THE OASIS OF HEALING MINISTRIES (OHM)

Yafuatayo ni maelezo mafupi ya vipengele muhimu vinavyohusiana na huduma ya The Oasis of Healing Ministries (OHM) iliyoko Ubungo, Dar es Salaam, Tanzania.  Inazungumzia mambo mengi yanayohusiana na OHM ikiwa ni pamoja na maono, kauli ya utekelezaji wa huduma (mission statement), historia yake, anwani yake na mahali OHM ilipo. Zaidi ya hayo haya maelezo yanaweka wazi vipengele vingine vya OHM ikiwa ni pamoja na maadili tunayoyasimamia (core values), ibada za kila wiki, matawi na makanisa ya OHM, vitabu vilivyoandikwa na Prosper Ntepa na Deborah Ntepa na Mashine ya Kuchapa Vitabu, mafanikio katika Huduma, Chuo cha Biblia cha The Oasis of Healing Bible College (OHBC), historia fupi ya Prosper na Deborah Ntepa na shuhuda za uponyaji na kufunguliwa. Maelezo haya yanatarajiwa kuwasaidia washirika wetu kuelewa vizuri kuhusu Oasis of Healing Ministries mahali ilikotoka, mahali ilipo sasa na kule inakoelekea kwa maana ya maono na mwelekeo wake.

 

MAONO YA THE OASIS OF HEALING MINISTRIES (OHM)

OHM itakuwa ni kisima cha uponyaji kwa wagonjwa wa aina zote waliookoka na wasiookoka na kuwa baraka kwa Mwili wa Kristo kwa njia ya kufundisha kusudi lote la Neno la Mungu.

 Watumishi wa Mungu wakihudumu pamoja na wachungaji Prosper na Deborah Ntepa kwa mshirika ambaye alipokea muujiza na bwana Yesu kumponya ugonjwa uliokuwa unamsumbua.

KAULI YA UTEKELEZAJI WA HUDUMA (MISSION STATEMENT)

Kuwaandaa na kuwafundisha waamini kufikia ukomavu wa kiroho, kuendeleza vipaji vya Kimungu walivyopewa kwa makusudi yake na kuwa kisima cha uponyaji kwa magonjwa yote kwa watu wa mataifa yote.

MIKAKATI YA KUTIMIZA MAONO NA MWELEKEO WA HUDUMA YA OHM

 1. Kwa kusisitiza mafundisho ya uponyaji kama vile jinsi ya kupokea uponyaji na jinsi ya kuponya wagonjwa.
 2. Kwa kuchapa vitabu mbalimbali ambavyo vitakuwa baraka kwa Mwili wa Kristo.
 3. Kwa kuwasaidia waamini wa OHM kuhusu umuhimu wa kuzijua karama zao na vipaji walivyopewa na Mungu.
 4. Kwa kusisitiza utendaji badala ya vyeo ndani ya makanisa yetu.
 5. Kwa kuufikia Mwili wa Kristo kwa njia ya vyombo vya habari kama vile redio, runinga, vitabu, magazeti, tovuti, WhatsApp, na nyinginezo.
 6. Kupanda makanisa katika Tanzania kwa kadiri Roho Mtakatifu atakavyotuongoza.
 7. Kuendesha semina na makongamano ndani na nje ya Tanzania.
 8. Kuwaandaa waamini kuwafikia waliopotea na kuwaleta kwa Kristo kwa njia ya kozi maalum ya uinjilisti.
 9. Kuwasaidia wenye magonjwa sugu na magonjwa yasiyoponyeka ikiwa ni pamoja na wale wenye UKIMWI wapokee uponyaji wao.
 10. Kuandaa na kutoa mafundisho kuhusiana na jinsi ya kukua kiroho, kujua urithi wako Ndani ya Kristo kupitia kweli za Ndani Yake na kuwasaidia waamini kuzijua ahadi za Neno la Mungu.
 11. Kuwa na kanisa kubwa katika makao makuu ya huduma ya OHM ya Ubungo wa Dar es Salaam.
Advertisements

Powered by WordPress.com.

Up ↑

%d bloggers like this: