IBADA/MATAWI

IBADA ZA KILA WIKI ZA KANISA LA OHM

s5000196

Tunazo ibada zifuatazo kila wiki: Kila Jumapili tunazo ibada mbili: ibada ya kwanza inaanza saa 1:30 hadi saa 4.00 asubuhi. Ibada hii huendeshwa kwa lugha mbili; huendeshwa kwa Kiingereza na kutafsiriwa kwa Kiswahili. Ibada ya pili ni ya Kiswahili na inaanza saa 4.00 asubuhi hadi saa 7.30 mchana. Tunayo ibada ya katikati ya juma siku ya Alhamisi kuanzia saa 10.00 hadi saa 12.30 jioni ambapo jumbe zinazohusu uponyaji, kufunguliwa, imani na masomo yanayoendana na hayo hufundishwa. Siku za Ijumaa kuanzia saa 10.00 jioni hadi saa 2.00 usiku tunafanya maombi na kuombea ujazo wa Roho Mtakatifu. Jumatano ya kila wiki tuna ushauri wa mtu mmoja mmoja, maombezi kwa ajili ya uponyaji na kufunguliwa kuanzia saa 5.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni. Pia kuna ushauri, maombi ya uponyaji na kufunguliwa siku ya Alhamisi kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 10.00 jioni na pia Jumapili kuanzia saa 7.30 hadi saa 8.00 mchana yaani mara tu baada ya ibada ya pili.

 

MATAWI NA MAKANISA YA OHM

Huduma ya Oasis  of Healing Ministries ina matawi mengi ikiwa ni pamoja na 5 yaliyoko Dar es Salaam. Tawi la kwanza lilipandwa Magomeni Kagera tarehe 22 Machi 2006 na Mchungaji Bahati Nyagawa ila kwa sasa limehamishiwa Ulongoni, Gongo la Mboto mwezi Agosti 2014. Matawi mengine yaliyoko Dar es Salaam pamoja na majina ya wachungaji wao katika mabano ni pamoja na: Makoka (Mch. John Mikowelo), Kinyerezi (Mch. Ibrahimu Matola), Mbagala (Mch. Dismas Lyanga), Mburahati (Mch. Erick Kiwia). Pia tunalo tawi mkoani Mbeya ambalo lilianzishwa tarehe 28 Machi 2010 chini ya uongozi wa Mtume Prosper Ntepa ambaye aliongozwa ampeleke Mchungaji Michael Wanzagi. Mchungaji aliyeko Mbeya kwa sasa hivi ni Evance Emmanuel. Mipango iko mbioni kupanda makanisa katika mikoa ya Dodoma, Arusha na Morogoro. Tarehe 3 Januari 2017 Mungu alisema na mchungaji Prosper Ntepa kuanza kupanda kanisa moja kila mwaka. Kuanzia Mei 2017 tupanda kanisa Dodoma.

 

MAFANIKIO KATIKA HUDUMA

Kuna mambo mengi ambayo tumefanikiwa kuyafanya kwa neema ya Mungu. Tumefanikisha mambo mengi: Kwanza kuna mafanikio mengi katika huduma ya uponyaji. Mamia ya watu wameponywa magonjwa na maumivu kupitia huduma yetu. Tumeshuhudia uponyaji wa namna mbalimbali kwa magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na upofu, uziwi, utasa, magonjwa yasiyoponyeka kama vile saratani, UKIMWI, vidonda vya tumbo. Kumekuwa na miujiza zaidi ya mia moja ya kufutika kwa alama za mishono ya wale waliojifungua kwa operesheni. Zaidi ya watu 50 wameponywa UKIMWI kwa njia ya maombi.

Pili, kuna mafanikio mengi katika upande wa machapisho ikiwa ni pamoja na vitabu. Mchungaji Prosper Ntepa amekuwa ni mwandishi wa vitabu vingi. Mpaka sasa ameshaandika vitabu 40 kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Hata hivyo kuna vitabu vingi zaidi ya hivyo ambavyo vimo kwenye kompyuta vikisubiri kuchapwa kuliko vile ambavyo vimeshachapwa.

Mchungaji Prosper Ntepa anasema, “Nimekuja kugundua kwamba kipawa cha kuandika vitabu vya Kikristo ni mojawapo ya neema kuu ambazo Mungu ameziweka ndani yangu. Kuna wakati ninashangazwa kuona jinsi utajiri wa neema hii ulivyo mwingi kwangu. Hii ilikuwa ndiyo sababu ya kuanzishwa kwa kampuni ya Prosper Printing Company.”

Tatu, kuna mafanikio mengi katika huduma ya kufundisha. Kwa neema ya Mungu huduma yetu ya kufundisha imewagusa maelfu ya watu wengi kupitia vitabu, semina, makala za magazetini za kila wiki na huduma kwa njia ya redio.

Nne, kuna mafanikio mengi katika kazi ya kuwafundisha watumishi wa Mungu. Hii imekuwa ni sehemu ya huduma ya utume wa Prosper Ntepa. Mtume Prosper Ntepa ni mwalimu wa waalimu kwa maana ya kwamba amekuwa akiwaandaa wale ambao wamekuwa wakifundisha katika Mwili wa Kristo. Huduma hiyo ya kitume ni pamoja kuwaandaa na kuwafundisha watumishi kwa ajili ya kazi ya huduma.

Tano, tumeona mafanikio katika uandishi wa mashairi na ushairi. Mchungaji Prosper Ntepa kama mshairi ameshaandika mashairi ya Kiingereza zaidi ya 100.

Sita, tumeweza kujenga jengo la kanisa ambalo lina uwezo wa kuketisha watu zaidi ya 700. Kuanzia mwezi Desemba 2016 jengo hili lilianza kukarabitiwa ili kuweka ceiling  board na kiyoyozi.

Saba, tunazo hekari kama tatu huko Kerege, Bagamoyo ambapo tuna mpango wa kujenga shule ya Biblia na shule ya Sekondari ya kimataifa.

Advertisements

Powered by WordPress.com.

Up ↑

%d bloggers like this: