POSTS

Books/magazine, Deborah's teachings

JINSI YA KUPOKEA UPONYAJI WA “MOYO ULIOUMIZWA” na mch. DEBORAH NTEPA

JINSI YA KUPOKEA UPONYAJI WA “MOYO ULIOUMIZWA”:

Ikiwa umeshindwa kuulinda moyo wako kwa sababu ya kuzidiwa na mambo magumu na mabaya sana; usikate tamaa, bado tumaini lipo. Wengi hudhani kwamba upako wa Roho Mtakatifu ni kwa ajili ya kuhubiri habari njema na kuombea wagonjwa tu. Lakini Neno la Mungu linaonyesha wazi kwamba kuna upako wa kuganga mioyo iliyovunjika. Isaya 61:1 inasema, “Roho ya Bwana Mungu i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo. Lipo tumaini la kupata uponyaji wa moyo uliovunjika. Kama Neno la Mungu linavyosema. Upo upako wa kuganga moyo uliovunjika. Uponyaji wa moyo ulioumizwa huambatana na uponyaji wa magonjwa yanayotokana na kuumizwa moyo. Njia zifuatazo zinaweza kukusaidia kupata uponyaji wa moyo wako

1. Kumwomba Mungu

Kama vile mgonjwa anavyomwomba Mungu kwa ajili ya uponyaji wa magonjwa, ndivyo unaweza kumwomba Mungu akuponye moyo wako. Kuna upako maalum wa kuponya mioyo iliyoumia. Haijalishi umeumizwa kiasi gani, Mungu ana uwezo wa kukuponya. Zaburi 147:3 inasema, “Huwaponya waliopondeka moyo na kuziganga jeraha zao.”

Continue reading “JINSI YA KUPOKEA UPONYAJI WA “MOYO ULIOUMIZWA” na mch. DEBORAH NTEPA”

Books/magazine, Deborah's teachings

MCH DEBORAH AMEANDIKA KITABU HIKI KWA LUGHA NNE SASA!

“Asante Mungu wa OHM” ndivyo unavyoweza kusema kutokana na kazi njema anayofanya mtumishi wa Mungu Mchungaji Deborah Ntepa. Kwa miaka mingi sasa, Mungu amekuwa akimtumia kwa njia nyingi ikiwemo uandishi wa vitabu. Moja ya kitabu ambacho kimeendelea kuwa “kitabu pendwa” ni kinachoitwa UPONYAJI WA MOYO ULIOUMIZWA. Kitabu hiki kimekuwa baraka sana na uponyaji kwa watu wengi ndani na nje ya Tanzania.  Continue reading “MCH DEBORAH AMEANDIKA KITABU HIKI KWA LUGHA NNE SASA!”

shuhuda

DADA “S” APONYWA UKIMWI KWA HARAKA SANA

DADA “S” APONYWA UKIMWI KWA HARAKA SANA

  

Swali: Uliokoka lini?                                                             

Jibu: Niliokoka tarehe 12 Julai 2006.

 Swali: Ulipima lini na ukajua kuwa umeathirika?

Jibu: Nilipimwa tarehe 11 Agosti 2006.

Nilipopimwa sikukata tamaa tarehe 12 Julai 2006 ndipo nikaamua kuokoka kwa sababu niliamini kuwa Mungu anaweza kuniponya, neno likanijia kuwa usikate tamaa muujiza wako uko njiani, nikajipa moyo, sikukata tamaa, japokuwa nilipata taabu niliporudi nyumbani moyo ukawa unaniuma sana mawazo mengi yakanisonga, lakini nikaendelea kujipa moyo kwani niliamini kuwa siku moja Mungu ataniponya.

Niliendelea kumwomba Mungu japokuwa sikuwa na neno sana la kunipa moyo. Kwa hiyo mimi nikaendelea kuomba tu.

Nilikuwa na mazoea ya kusikiliza redio (Upendo Redio).  Siku moja kulikuwa na mwinjilisti mmoja akawa anafundisha juu ya kuwa Mungu anaweza kuponya magonjwa yote, nikapiga simu na kuelezea matatizo niliyokuwa nayo, dada mmoja ambaye anafanya kazi hapo redioni akaniita, nikaenda akanitia moyo na kuniambia kuwa nitakupeleka  kanisani ukaombewe na kusikiaNeno la kusimamia katika hilo tatizo lako. Continue reading “DADA “S” APONYWA UKIMWI KWA HARAKA SANA”

Poems, Prosper Teachings

UNAPASWA KUJUA JINSI YA KUFANIKIWA(SHAIRI) Na Mhungaji PROSPER NTEPA

SHAIRI LA UNAPASWA KUJUA JINSI YA KUFANIKIWA (YOU MUST KNOW

HOW TO SUCCEED)

PROSPER NTEPA

 

Badili namna unavyofikiri,

Maana mawazo yako yakishibishwa fikra za umaskini,

Maisha ya mafanikio yanakuwa kama mtu anayeota ndoto za mamilioni ya dola,

Kisha akiamka ni maskini anayechukia kila kinachomzunguka.

 

Fanya kazi kwa bidii katika mambo yako,

Maana ukikumbatia uvivu,

Unakuwa kama gari lililonasa katika matope,

Ambalo haiwezekani kuliendesha litoke.

 

Badili tabia yako, Continue reading “UNAPASWA KUJUA JINSI YA KUFANIKIWA(SHAIRI) Na Mhungaji PROSPER NTEPA”