Our Products

VITABU VILIVYO ANDIKWA NA WACHUNGAJI PROSPER NTEPA NA DEBORAH NTEPA

  1. FUNGUO SABA ZA KUKUSAIDIA KUJIFUNZA KUTOA UNABII;

Kitabu hiki ni ufunuo wa kukusaidia kutembea katika karama tisa za roho mtakatifu. Lengo la kitabu hiki sio kutoa nadharia juu ya karama za roho mtakatifu bali ni kufundisha namna ya kutembea katika karama za roho mtakatifu. Mwandishi wa kitabu hiki ana uzoefu wa kutembea katika karama za roho mtakatifu kama aina za lugha, tafsiri za lugha, unabii, neno la maarifa, kupambanua roho, neno la hekima, na karama za uponyaji. Mtume Prosper Ntepa anaamini kuwa kitabu hiki kitawasaidia wakristo wengi waliojazwa roho mtakatifu kunena lugha za ujumbe, kutoa tafsiri, kutoa unabii na kusikia sauti ya MUNGU.

Kinapatikana katika duka la kanisa la vitabu lililopo kanisani pale OHM-UBUNGO, Nyuma ya UBUNGO PLAZA karibu na shule ya msingi UBUNGO NATIONAL HOUSING. AU piga 0713212440/0767212440.

Kwa mliopo mikoani, vinawezwa kutumwa ukiweka order yako. Piga namba hapo juu.

Nyote mnakaribishwa…

………………………………………………………………………………………………

      2. JINSI YA KUJIANDAA KUOA NA KUOLEWA.

Kitabu hiki kitawasaidia wanaume na wanawake katika kupata mwenzi sahihi katika maisha yao. Maandalizi ya kuoa na kuolewa ni eneo muhimu sana linalohitaji uangalifu na hekima. Kuoa ni mojawapo ya mambo ambayo hayahitaji kukurupuka na kufanya haraka. Inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 50 ya mafanikio katika ndoa yanaanzia na chaguo sahihi la mwenzi sahihi yaani mke au mume sahihi. Pia inakadiriwa kuwa asilimia 50 ya ndoa mbaya zilizojaa machungu na migogoro zinaanzia na chaguo lisilo sahihi la mke au mume.

Kinapatikana katika duka la kanisa la vitabu lililopo kanisani pale OHM-UBUNGO, Nyuma ya UBUNGO PLAZA karibu na shule ya msingi UBUNGO NATIONAL HOUSING. AU piga 0713212440/0767212440.

Kwa mliopo mikoani, vinawezwa kutumwa ukiweka order yako. Piga namba hapo juu.

Nyote mnakaribishwa…

 ……………………………………………………………………………………………….

Advertisements

Powered by WordPress.com.

Up ↑

%d bloggers like this: